| WELCOME TO | ||
| MADRASA AL-HIDAYA | ||
| MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE | 
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)  
HAKI ZA JIRANI 
Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar (ر ) na Bi Aisha (ر ) kuwa walisema Mtume (ص ) amesema “Malaika Jibril aliendelea kuniusia haki za jirani hata mikadhani kwamba jirani atapata haki za kurithi”. (Bukhari na Muslim)
- Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (ر ) kuwa alimuuliza Mtume (ص ) “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nina majirani wawili, jee ni nani kati yao nimpe tunu”. Akasema, “mpe ambaye mlango wake uko karibu sana na mlango wako”. (Bukhari)
- Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema “Enyi wanawake wa Kiislamu, msidharau mmoja wenu kumpelekea jirani yake chochote kidogo japokuwa ni muundi wa mbuzi”. (Bukhari na Muslim)