Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

WEPESI KATIKA DINI

  1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Masoud (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Wameangamia na kupotoka wenye kuweka mikazo zaidi katika ibada zao”. Na alisema hayo mara tatu. (Muslim)
  2. Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (ر ) kuwa alisema, “Mtume (ص) alikuwa akiacha kufanya jambo ingawaje apenda kulitenda, kwa hofu watu (waislamu) watalitenda kisha wakalifanya liwe faradhi juu yao”. (Bukhari na Muslim)
  3. Imepokewa kutoka kwa Bin Umar (ر ) kuwa alisema, “Tulikuwa tunapombai Mtume (ص) (kuapa juu ya utiifu) kwa kumsikiza na kumtii, alikuwa akituambia, “kwa kadiri mnavyoweza”. (Bukhari na Muslim)
  4. Impekewa kutoka kwa Anas Bin Malik (ر ) kuwa Mtume (ص ) alisema, “Yafanyeni mambo kuwa sahali na yanayowezekana na wala musiyafanye magumu.  Muwabashirie watu (kuhusu mazuri yatakayotokea) na wala msiwafanye wawe na chuki”. (Bukhari na Muslim)

 

 

 


 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS